3 Mei 2025 - 23:17
Source: Parstoday
Qamati: Ni upuuzi na maneno matupu kutaka Hizbullah ipokonywe silaha

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imesema kuwa, adui ana hofu kubwa na silaha za muqawama na kwamba, ni maneno ya kipuuzi na yasiyo na maana kutaka harakati hiyo ipokonywe silaha.

Hayo yameelezwa na Mahmoud Qamati, Naibu Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah na kusisitiza kwamba, wito wa kutaka harakati hiyo ipokonywe silaha ni maneno yasiyo na faida yoyote.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Hizbullah ameongeza kuwa, kutokana na kusimama kidete kusiko na mithili na kwa ushupavu kwenye mipaka, na vilevile kulindwa nguvu ya Lebanon kwa stratijia ya pande tatu, adui Mzayuni alishindwa kuunda Mashariki ya Kati mpya.

Aidha amesema: "Tumewapoteza viongozi wetu wapenzi, wakiongozwa na shahidi Sayyed Hassan Nasrullah. Sasa wanataka kuchukua silaha za muqawama bila ya gharama yoyote. Hii haimaanishi kwamba tunataka kutoa silaha zetu kwa gharama fulani."

Hapo awali, Nabih Berri, Spika wa bunge la Lebanon alisema: "Silaha yetu ni turufu ambayo hatutaacha bila ya kutekelezwa

Qamati: Ni upuuzi na maneno matupu kutaka Hizbullah ipokonywe silaha

kikamilifu kwa usitishaji vita na kuzungumza juu ya hatima ya silaha hii."

Spika Berri amekaribisha kwa mikono miwili na kueleza kuridhishwa kwake na mazungumzo kati ya Rais wa Lebanon Joseph Aoun na Hiziollah, maoni yake kuhusu harakati hiyo ya muuqawama.

 "Lakini pia ni muhimu kuweka shinikizo kwa adui kutimiza majukumu yake chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano," Berri aliongeza.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha